Tarehe: 7 Novemba 2026
Karibu Madeni. Kwa kutumia mfumo huu, unakubaliana na masharti yafuatayo:
Kuweka kumbukumbu za madeni, malipo, orodha ya wateja, na kutoa taarifa za CSV ni bure daima. Malipo yanahusika tu unaponunua SMS credits za kutuma kumbusho.
Wewe kama mwenye duka unawajibika kuhakikisha madeni unayorekodi ni halisi na namba za simu unazoweka ni za wadaiwa wako halali. Hairuhusiwi kutumia mfumo huu kumsumbua mtu asiyekuwa mdaiwa wako.
Madeni inatumia lugha ya heshima na haina jumbe za vitisho au kuudhi. Mfumo unazingatia muda wa kazi (saa 2:00 asubuhi hadi 1:00 jioni) na haumsumbui mteja mara nyingi kwa siku.
© 2026 Madeni by SendAfrica. Haki zote zimehifadhiwa.